<?xml version="1.0" encoding="UTF-8"?><song><hymn_number>99</hymn_number>
<lyrics>[V1]
 Maelfu na maelfu
 Wenye nguo bora!
 Masafu ya waongofu
 Wenye na bendera!
 Amekwisha kamili
 Vita vya shetani
 Fungueni lango hili;
 Njoni, ingieni!

[V2]
 Imbeni aleluya,
 Zipae Mbinguni!
 Pigeni sana sauti
 Kwa kutumaini!
 Kwa hiyo viliumbwa
 Nchi hata Mbingu
 Dhiki za muda zikisha,
 Asifiwe Yesu.

[V3]
 Loo! Tukionana
 Pwani ya ng'amboni!
 Loo! Tukishirikiana
 Milele Mbinguni!
 Midomo yote pia,
 Huko itaimba
 Wajane kufufukiwa
 Na kila yatima!

[V4]
 Himiza enzi yako,
 Uliyetufia
 Utimize watu wako,
 Wakosaji pia,
 Mpendwa wa taifa
 twakutumaini!
 Uzifunue ishara
 Urudi enzini!</lyrics>
<title>Maelfu Na Maelfu TZR99</title>
</song>